Tuesday , 28th Jul , 2015

Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru mwaka huu,Juma Khatib Chuma amewataka Watanzania kutumia uchaguzi mkuu wa mwaka huu kuwaweka madarakani viongozi watakaoweza kuwasaidia wananchi kuondokana na kero mbalimbali bila kujali itikadi ya vyama vya siasa.

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Luten Kanali Mstaafu Issa Machibya.

Akizungumza na wananchi wa tarafa ya Nguruka mara baada ya Mwenge wa Uhuru kuanza mbio zake mkoani Kigoma baada ya kumaliza mkoani Tabora , amesema watanzania wasiwape nafasi wagombea watakaokuja na sera za kuwagawa watanzania na kuhatarisha amani na kwamba wawaepuke viongozi watakaotumia rushwa kununua uongozi.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Kigoma Luten Kanali Mstaafu Issa Machibya akizungumza baada ya kupokea mwenge wa uhuru kutoka kwa kaimu mkuu wa mkoa wa Tabora Seleman Kumchaya amesema miradi yenye gharama ya zaidi shilingi bilioni 19 itazinduliwa na kuwekewa mawe ya msingi katika halmashauri saba za mkoa wa kigoma.

Aidha viongozi wa mikoa hiyo wameeleza kushindwa kufikia malengo ya uandikishaji wapiga kura katika mikoa ya Tabora na Kigoma