Kupitia mtandao wa X Mbunge na Waziri wa zamani wa Ardhi, Prof. Anna Tibaijuka amesema uamuzi wa Rais wa Marekani Donald Trump kusitisha misaada kwa mashirika ya afya duniani kama GLOBAL FUND iwapo yatatekelezwa ni kiama.
"Upatikanaji wa madawa ya kuongeza kinga za mwili ARVs utaathirika. Ninashauri Wizara ya Afya kuufahamisha umma wa waTanzania je ni hatua gani za haraka zinachukuliwa kutathmini jambo hili na kuchukua hatua stahiki?."
"Ikibidi African Union waitishe kikao maalum kuangalia swala hili na kuweka mkakati wa pamoja. Waathirika wa gonjwa hili la UKIMWI ni waAfrika na ugonjwa haujulikani ulitoka wapi?. Tujitetee."
"Aidha juhudi za kuthibiti maambukizi ya virus vya ukimwi ziwekewe nguvu mpya. Upatikanaji wa ARVs utakuwa mgumu. Na kununua ARVs kibiashara ni jambo litakalohitaji bajeti kubwa na uwezo wa taifa kwa ujumla ni mdogo. Na jambo limekuwa la ghafla. Waathirika wengi hawana uwezo kununua madawa hayo wenyewe maisha yao yote. Afya zao zikidhoofika itatumika gharama kubwa kuwauguza hivo kusababisha umaskini na vifo. Pia bila ARVs maambukizi yatashika kasi mpya. Tuwe macho"