Monday , 6th Jan , 2025

Timu ya Simba SC imeshinda mchezo wa kombe la shirikisho ugenini nchini Tunisia dhidi ya timu ya CS Sfaxien kwa goli 1-0 lililofungwa na Kiungo wa ushambuliaji raia wa Ivory Coast Jean Charles Ahoua.

Timu chache ndani ya hii miaka mitano ya hivi karibuni zimeweza kuwa na muendelezo mzuri wa kushiriki michuano ya Afrika na kufika hatua ya robo fainali ya mashindano hayo kama Simba SC.

Timu ya Simba SC imeshinda mchezo wa kombe la shirikisho ugenini nchini Tunisia dhidi ya timu ya CS Sfaxien kwa goli 1-0 lililofungwa na Kiungo wa ushambuliaji raia wa Ivory Coast Jean Charles Ahoua.

Ushindi huo umeifanya timu hiyo yenye masikani yake mtaa wa Kariakoo kufikisha alama 9 ishika nafasi ya pili katika msimamo wa kundi A linaloongozwa na timu ya CS Constantine ya nchini Algeria.

Simba SC inapambana kufuzu hatua ya robo faianli yake ya 6 nne zikiwa za kombe la klabu bingwa Afrika na mbili zitakuwa za shirikisho Afrika. Mashabiki wa kikosi cha Wekundu wa Msimbazi wanaimani kubwa na timu yao msimu huu kuvuka hatua ya robo fainali na kucheza nusu fainali ya kombe la shirikisho Afrika.

Timu inayonolewa na Kocha raia wa Afrika ya kusini ni moja kati ya vikosi vinavyoangaliwa kwa ukaribu na Wadau wa Soka Afrika na inapigiwa chepuo kufika fainali au kuchukua kabisa kombe msimu huu. Kuna Wachezaji ambao wanauzoefu mkubwa wa michuano ya Africa kama Fabrice Ngoma, Shomari Kapombe,Mohamed Hussein na Moussa Camara.

Heshima iliyojijengea klabu ya Simba katika mashindano ya Afrika si kitu ambacho kinatakiwa kuchukuliwa kwa kawaida na hiyo ndiyo sababu ambayo Wachezaji wengi wanavutiwa kujiunga na timu hiyo ili kuonekana katika ulimwengu wa Soka la Afrika.

Timu chache ndani ya hii miaka mitano ya hivi karibuni zimeweza kuwa na muendelezo mzuri wa kushiriki michuano ya Afrika na kufika hatua ya robo fainali ya mashindano hayo kama Simba SC.

Kilichobaki kwa klabu hiyo mabingwa wa zamani wa ligi kuu Tanzania bara ni kuvuka hatua ya robo fainali na kuanzisha ukurasa mpya wa kucheza hatua ya nne bora ya mashindano ya CAF ili kujijengea heshima zaidi na kuogopwa.

Wapinzani wa Mnyama kama inavyojulikana na Wapenzi wa Soka Tanzania Wanahofia kucheza dhidi ya timu hiyo kwenye uwanja wake wa nyumbani wa Benjamini MKapa kutokana na matokeo yake inapocheza uwanja huo.

Ukanda wa Afrika ya Mashariki unaogopwa kwasasa kutokana na Simba SC kuuwakilisha vizuri ukanda huo.

Heshima iliyojingea klabu ya Simba haipaswi kubezwa bali kuigwa na timu nyingine ili kuliletea taifa la Tanzania heshima zaidi katika mashindano ya vilabu Afrika.