Thursday , 28th Nov , 2024

Kikosi cha Real FC Madrid siku ya jana kilijikuta kwenye wakati mgumu lilipocheza na timu ya Liverpool ya Uingereza katika mwendelezo wa michezo ya ligi ya mabingwa barani Ulaya kwa kupoteza mchezo huo kwa magoli 2-0 magoli yaliyofungwa na Alexis Mac Allister na Cody Gakpo.

Kipigo hiko kutoka kwa Liverpool kwenye uwanja wa Anfield kumeifanya Madrid kusalia na alama zake 6 baada ya kucheza michezo mitano inashika nafasi ya 24 katika mashindano yenye timu 36. Kikosi cha Los Blancos ndio mabingwa watetezi wa kombe la klabu bingwa barani msimu huu inakutana na wakati mgumu kutokana na kutokuwa kwenye kiwango chake kilichozoeleka katika mashindano ya msimu huu wenye mfumo tofauti na uliozoeleka

Kikosi cha Real FC Madrid siku ya jana kilijikuta kwenye wakati mgumu lilipocheza na timu ya Liverpool ya Uingereza katika mwendelezo wa michezo ya ligi ya mabingwa barani Ulaya kwa kupoteza mchezo huo kwa magoli 2-0 magoli yaliyofungwa na Alexis Mac Allister na Cody Gakpo yalitosha kupeleka kilio kwa Mashabiki wa Madrid wanaofahamika kwa jina la Madridistas.

Liverpool FC  ilitawala mchezo huo kwa muda mrefu na ilitengeneza nafasi nyingi za kufunga magoli lakini Washambuliaji wake walishindwa kuzitumia zote. Timu hiyo mabingwa wa kihistoria wa mashindano hayo usiku wa jana haikuwa na hatari yoyote mbele ya lango la Vijana Arne Slot pia haikutengeneza nafasi ya hatari ndani ya dakika 90 za mchezo mpaka Muamuzi alipotamatisha mchezo huo.

Wachezaji waliokuwa wakitazamiwa kufanya makubwa usiku wa jana Kylian Mbappé na Mohamed Salah walikosa penati walizopiga Mbappe penati yake ilidakwa na Golikipa huku Salah akipiga nje. Eduardo Camavinga alitolewa mchezoni baada ya kuumia misuli na kuongeza idadi ya majeraha kwenye kikosi cha Carlo Ancelotti ambacho kinawakosa Wachezaji wengi wa kikosi chake cha kwanza.

Kipigo kutoka kwa Liverpool kwenye uwanja wa Anfield kimeifanya Madrid kusalia na alama zake 6 baada ya kucheza michezo mitano inashika nafasi ya 24 katika mashindano yenye timu 36. Kikosi cha Los Blancos ndio mabingwa watetezi wa kombe la klabu bingwa barani msimu huu inakutana na wakati mgumu kutokana na kutokuwa katika kiwango chake kilichozoeleka katika mashindano ya msimu huu wenye mfumo tofauti na uliozoeleka.

Madrid imesaliwa na michezo mitatu ambayo inapaswa ishindo yote ili kupata nafasi ya kufuzu kucheza hatua ya mtoano ya klabu bingwa Ulaya kwa msimu huu wa 2024-2025.