Wednesday , 27th Nov , 2024

Klabu ya Yanga inapitia kipindi kigumu kwasasa kutokana na matokeo mabaya ambayo timu hiyo imekuwa ikiyapata siku za karibuni.Imepoteza michezo mitatu mfululizo kitu ambacho hakijazoeleka na Mashabiki pamoja na Wanachama wa timu hiyo.

Timu zinapopitia wakati mgumu huwa vitu vingi huwa vinabadilika maswali yanakuwa mengi kuanzia kwenye ubora wa benchi la ufundi mpaka namna Wachezaji wanavyojituma kwenye michezo wanayocheza. Kuna kipindi timu huwa zinapitia wakati mgumu kwa fomu yake kushuka Wachezaji wote wanakuwa wapo chini kiuchezaji inahitaji uwezo mkubwa wa Mwalimu kuweza kurudisha hali ya upambanaji kwenye kikosi chake kwa kuhakikisha ari kwa Mchezaji mmojammoja ili timu irejee kwenye hali ya kawaida.

Kuna sababu mbalimbali zinazofanya timu kushuka kiwango ya kwanza inaweza kuwa ni uchovu kwa Wachezaji kutokana na kutumika kwa muda mrefu, sababu ya pili inaweza ikawa ni kuridhika kwa Wachezaji baada ya kushinda ubingwa kwa mara kadhaa mfululizo hivyo kunakuwa na hali ya kutotamani mafaniko zaidi tatizo hili linaweza kutatuliwa kwa kusajili Wachezaji wenye njaa ya mafanikio ili kuwapa changamoto wale waliopo kwenye kikosi cha muda huo.Sababu ya tatu inaweza kuwa ni uwepo wa Wachezaji wengi ambao viawango vyao kiuchezaji vimefika mwisho hakuna kitu kipya wanaweza kuongeza badala ya grafu zao kiuchezaji kushuka hapa timu huwa nayumba na huitaji kuanza upya ili kujenga timu yenye ushindani.

Uongozi unapaswa kuwa makini sana kwenye kipindi hiki champito kutokana na presha ambayo watakuwa wanaipata kutoka kila sehemu upende wa Mashabiki wataulaumu uongozi katika baadhi ya maamuzi ambayo wameyafanya kuhusiana na kuondolewa kwa Kocha au usajili wa baadi ya Wachezaji, Kiongozi asipokuwa na uwezo mkubwa wa kusimamia kwenye msimamo wake atajikuta anayumbishwa na kushindwa kuisimamia timu.

Kuna kosa kubwa lilifanywa na Uongzoi wa kikosi cha Wanajangwani kutokana na kumfuta kazi aliyekuwa Kocha wake mkuu Muargentina Miguel Angel Gamondi baada ya kikosi hiko kupoteza michezo miwili dhidi ya Azam FC na Tabora United.Naamini matatizo ya Yanga SC yalipaswa kutafutiwa ufumbuzi na Gamondi kwa vile timu haikuwa kwenye nafasi mbaya katika msimamo wa ligi kuu Tanzania mpaka anafukuzwa kikosi chake ilikuwa inashika nafasi ya pili kwa alama moja nyuma ya Watani wao wa jadi Simba SC. Kufukuzwa kwake kazi inamaanisha kikosi hiko kimeanza upya kwa kumleta kocha mpya hivyo kila kitu kiakuwa kipya kwenye benchi la ufundi.

Kocha mpya wa timu hiyo mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania bara Sead Ramovic hajaanza vizuri kazi yake baada ya kupoteza mchezo wake wa kwanza kuusimamia kwa kufungwa goli 2-0 dhidi ya Al-Hilal ya kutoka Sudan mchezo wa ligi ya mabingwa barani Afrika kundi A. Maneno yameanza kuzungumzwa mtaani kuhusiana na uzoefu wa Ramovic kuongoza klabu kubwa kama ya Yanga kwa mlinganisho wa timu aliyokuwa anaifundisha hapo kabla ya TS Galaxy ya Afrika ya Kusini.

Uongozi wa Yanga unapswa kuwa na uvumilivu kipindi hiki kigumu ambacho wanapitia kila timu Duniani huwa inapitia hali ambayo timu yao inapitia kwasasa Manchester City ipo kwnye hali hii haikufukuza Mwalimu wameamua kuvumilia wakifahamu fika ni swala la muda tu kabla ya klabu hiyo aijarejea katika hali yake ya ushindi.

Uongozi wa Yanga SC unapswa kuwa makini wakiingia kwenye kelele za Mashabiki na watu wa nje ya klabu yao wanaweza kufanya tena makosa ambayo yataigharimu klabu hiyo ubingwa wake ambao inapambana kuutetea.