Tuesday , 26th Nov , 2024

Klabu ya Simba itacheza mchezo wa kwanza kombe la shirikisho barani Afrika hatua ya makundi dhidi ya F.C. Bravos do Maquis kutokea Angola kesho kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa.

Kikosi cha Wekundu wa Msimbazi kinajivunia historia nzuri kinapocheza uwanja wake wa nyumbani katika mashindano ya vilabu Afrika kombe la shirikisho na klabu bingwa. Katika mashindano haya ya shirikisho Simba SC imefanikiwa kufika hatua ya robo fainali msimu wa 2020-2021 ambapo iliondoshwa mashindanoni na timu ya Kaizer Chiefs kutokea Afrika ya kusini.

Klabu ya Simba itacheza mchezo wa kwanza kombe la shirikisho barani Afrika hatua ya makundi dhidi ya F.C. Bravos do Maquis kutokea Angola kesho kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa. Kikosi cha Kocha Fadlu Davies kilifanikiwa kuingia hatua ya makundi kombe la shirikisho baada ya kuitoa timu ya Al Ahli SC ya nchini Libya kwa kuifunga magoli 3-1.

Kikosi cha Wekundu wa Msimbazi kinajivunia historia nzuri kinapocheza uwanja wake wa nyumbani katika mashindano ya vilabu Afrika kombe la shirikisho na klabu bingwa. Katika mashindano haya ya shirikisho Simba SC imefanikiwa kufika hatua ya robo fainali msimu wa 2020-2021 ambapo iliondoshwa mashindanoni na timu ya Kaizer Chiefs kutokea Afrika ya kusini.

Mchezo wa kesho ni muhimu kwa kikosi hiko kuanza na ushindi ili kujenga hali ya kujiamini kutokana na usajili wa Wachezaji wengi Vijana wenye vipaji vikubwa vya kucheza mpira wa miguu lakini hawana uzoefu wa kucheza mashindano ya vilabu barani Afrika. Ujio wao ndani ya Simba SC kumeongeza ubora wa timu yao pia kumeamsha matarajio mapya kwa Mashabiki na Wapenzi wa Wekundu wa Msimbazi.Malengo ya klabu hiyo msimu huu ni kuhakikisha inavuka hatua ya robo fainali ambayo imekuwa ikiishia mara kwa mara kwenye mashindano ya CAF.

Matarajio wa Viongozi wa mabingwa hao wa zamani wa ligi kuu Tanzania bara ni kurejesha ubingwa wao wa ligi kuu ya Tanzania bara ambao wameupoteza kwa miaka mitatu mfululizo mbele ya Watani wao wa jadi timu ya Yanga SC.Presha imekuwa kubwa kwa viongozi baada ya kupoteza utawala wake ndani ya Tanzania pamoja na kufanya makosa mengi ya usajili katika madirisha ya usajili yaliyopita.

Kocha mpya wa timu ya hiyo Fadlu Davies anatakiwa kuijenga timu kwa haraka ili iweze kushindania makombe yote inayoshiriki msimu huu.Mchezo wa kesho unaweza kutoa taswira ya kitu gani Simba SC inaweza kufanya kwenye kundi A lenye timu za F.C. Bravos do Maquis, CS Constantine, CS Sfaxien na Simba SC.

Simba SC ikifanikiwa kuvuka kucheza robo fainali itakuwa robo fainali yake ya pili ya kombe la shirikisho na itakuwa ya sita kwenye mashindano yote ya CAF kwa upande wa vilabu katika historia ya klabu hiyo.