Tuesday , 26th Nov , 2024

Hii siyo ngeni kwa wengi, kwani imekuwepo kwenye mtandao wa WhatsApp kwa muda mrefu hivi sasa lakini ni mpya kwa mtandao wa Instagram.

 

''Share your location'' ni feature mpya ambayo inamuwezesha mtumiaji wa Instagram kumjulisha na kumfahamisha jamaa au rafiki eneo ambalo upo kwa muda husika, 

Kikubwa kwenye ''Feature'' hii ni kwamba utaweza kuweka ukomo wa muda kwa maana unahitaji rafiki yako aone location yako kwa muda gani na baada ya hapo Location inatoweka

Na mtu ambaye utamtumia uelekeo uliopo ni miongoni mwa wale rafiki zako kwenye mtandao huo au kwenye groups ambazo wewe upo, na kwa usalama zaidi instagram wamezuia location yako ambayo ume'share kutumwa kwa mtu mwingine.

Kwa maana fupi itakuwa  ni kati ya pande mbili, mtu wa tatu hatoweza kufahamu uelekeo ambao umemtumia rafiki au group la washkaji zako.