Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Deus Sangu
wa miradi inayowanufaisha walengwa wa mfuko huo.
Mhe.Sangu ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kwela Mkoani humo ametoa pongezi hizo leo kwa nyakati tofauti wakati alipotembelea kukagua baadhi ya miradi inayotekelezwa na TASAF katika wilaya Nkasi na Kalambo.
Ameitaja miradi hiyo inayotekelezwa na TASAF ikiwemo ujenzi wa kisima cha maji katika wilaya ya Nkasi pamoja na uanzishwaji wa shamba la miti ya mbao Wilayani Kalambo.
Akizungumzia suala la ujenzi wa kisima hicho uliogharimu zaidi ya Sh.Milioni tatu hadi kukamilika kwake kimekuwa msaada mkubwa kwa kuhudumia zaidi ya kaya 200 katika Kijiji cha Kantawa
"Jambo kubwa lililonileta hapa ni kufuatilia utekelezaji wa fedha za mradi wa TASAF , mfuko huu umekuwa na programu mbalimbali, zikiwemo zile zinazolenga kaya maskini ambazo hupokea fedha, pamoja na shughuli za kujitolea ikiwemo ujenzi wa hiki kisima ambapo nimefarijika mno kujionea jinsi wananchi wanavyoisaidika kupitia kisima hiki," amesisitiza Mhe. Sangu