Carsley alichukuwa nafasi ya aliyekuwa Kocha wa timu hiyo Gareth Southgate aliyejiuzulu baada ya michuano ya UEFA Euro 2024. Ameiongoza timu hiyo michezo sita akifanikiwa kushinda michezo mitano na kupoteza mmoja dhidi ya Ugiriki uliofanyika mwezi Oktoba 2024.
Kaimu Kocha mkuu wa timu ya taifa ya England Lee Carsley amemaliza muda wake wa kufundisha timu ya taifa hilo kwenye mchezo dhidi ya Ireland ambao umetamatika kwa kikosi cha Simba watatu kushinda kwa ushindi mnono wa goli 5-0 ushindi huo umeifanya England kufuzu kucheza Ligi A ya mataifa ya bara la Ulaya.
Carsley alichukuwa nafasi ya aliyekuwa Kocha wa timu hiyo Gareth Southgate aliyejiuzulu baada ya michuano ya UEFA Euro 2024. Ameiongoza timu hiyo michezo sita akifanikiwa kushinda michezo mitano na kupoteza mmoja dhidi ya Ugiriki uliofanyika mwezi Oktoba 2024.
Thomas Tuchel anatarajiwa kuanza kazi ya kufundisha kikosi hiko cha mabingwa wa kombe la Dunia wa mwaka 1966 fainali zilizofanyika nchini humo tarehe 1 January 2025.Mkataba wake utafika kikomo baada ya kombe la Dunia la mwaka 2026 zitakazofanyika kwa uandaaji wa pamoja nchi za Marekani,Canada na Mexico.
Tuchel raia wa Ujerumani anakuwa Kocha wa tatu ambaye si Muingereza kufundisha timu pendwa na Waandishi wa habari. Anafata nyayo za Sven-Göran Eriksson raia wa Sweden na Muitaliano Fabio Capello ambao wote walishindwa kuipa mafanikio kimataifa timu hiyo.
Matumaini yamekuwa makubwa kwa Shirikisho la mpira England uwepo wa Mjerumani huyo kunaweza kuipatia kombe lolote la mashindano makubwa iwe kombe la Dunia, UEFA Euro ama UEFA European Football Championship ( Kombe la ligi ya mataifa ya Ulaya ).
Lee Carsley kabla ya kukaimu nafasi ya Ukocha mkuu timu ya taifa ya wakubwa England alikuwa anafundisha timu ya vijana chini ya umri wa miaka 21 ya taifa hilo, baada ya majukumu yake kutamatika rasmi siku ya jana atarejea kwenye majukumu yake ya awali na ameonyesha kufurahishwa kuifundisha England ya wakubwa japo kwa hiyo michezo sita pekee.