Nyota huyo wa zamani wa VfL Wolfsburg na Borussia Mönchengladbach anatarajiwa kufanya makubwa kikosi cha Yanga FC kutokana na kurithi kikosi chenya Wachezaji bora walio washindani.Kazi yake ya kwanza itakuwa kurudisha viwango vya Wachezaji vilivyoporomoka, pili kusimamia nidhamu za Wachezaji wa kikosi hiko kutokana na kuvuja kwa taarifa kuhusiana na nyota wengi wa mabingwa hao watetezi wa ligi kuu Tanzania bara kuendekeza starehe na kuporomosha viwango vyao.
Sead Ramovic anaweza kutangazwa muda wowote kuanzia sasa klabu ya Yanga SC kuwa Kocha mpya wa timu hiyo baada ya kumfukuza kazi aliyekuwa Kocha wake Miguel Gamondi kutokana na mwenendo mbovu wa timu hiyo klabu kwenye ligi kuu Tanzani bara baada ya kupoteza michezo miwili mfululizo dhidi ya Azam FC na Tabora United.
Ramovic alikuwa akiifundisha timu ya TS Galaxy ya Afrika ya Kusini ameshawasili Tanzania tangu jana usiku kinachosubiriwa ni kutangazwa tu kuwa Kocha wa Wanajangwani.Kocha huyo raia wa Ujerumani anauzoefu mkubwa wa kufundisha mpira Afrika hivyo ujio wake ndani ya Jangwani hautokuwa na shida kuzoea mazingira pamoja na Wachezaji.
Nyota huyo wa zamani wa VfL Wolfsburg na Borussia Mönchengladbach anatarajiwa kufanya makubwa kikosi cha Yanga FC kutokana na kurithi kikosi chenya Wachezaji bora walio washindani.Kazi yake ya kwanza itakuwa kurudisha viwango vya Wachezaji vilivyoporomoka, pili kusimamia nidhamu za Wachezaji wa kikosi hiko kutokana na kuvuja kwa taarifa kuhusiana na nyota wengi wa mabingwa hao watetezi wa ligi kuu Tanzania bara kuendekeza starehe na kuporomosha viwango vyao.
Mafanikio makubwa ya Ramovic akiwa TS Galaxy akiwezesha kikosi hiko kumaliza nafasi ya sita ligi kuu ya Afrika ya Kusini pamoja na kucheza hatua ya fainali kombe la Carling Knockout ikapoteza dhidi ya Stellenbosch.
Yanga SC imashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu Tanzania bara ikiwa imejikusanyia alama 24 baada ya kucheza michezo 10 ya ligi alama moja nyuma ya Simba SC inayoongoza msimamo ikiwa na alama zake 25 kumfuta kazi Gamondi ikiwa timu ipo nafasi ya pili tena ikizidiwa alama 1 tu na anayeongoza ligi inahitaji ujasiri mkubwa kwa Viongozi wa Yanga.
Taarifa ambazo si rasmi na bado kuthibitishwa na Uongozi wa timu ya Wananchi ni kuhusiana na Kocha mpya na msaidizi wake huku zikimuhusisha aliyekuwa Mkufunzi wa KMC FC Abdihamid Moalin kujiunga na kikosi hiko kuwa msaidizi wa Sead Ramovic.
Vyovyote itakavyokuwa Yanga SC imeamua kuanza upya kwa kumfuta kazi Gamondi na msaidizi wake Moussa N'Daw ili kukijenga upya kikosi ambacho kinapambana kutetea ubingwa wake wa ligi kuu Tanzania bara na kombe la shirikisho sambamba na kufanya vizuri mashindano ya klabu bingwa Afrika kuanzia mchezo wa tarehe 26, 2024 dhidi ya Al- Hilal Omdurman ya Sudan.