Stars inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa kundi H ikiwa na alama zake 4 baada ya kucheza michezo minne ikishinda mechi moja ikitoka suluhu mechi moja na kupoteza michezo miwili mfululizo dhidi ya timu ya taifa ya Congo DRC.
Timu ya taifa ya Tanzania taifa Stars itacheza mchezo wa kufuzu AFCON 2025 dhidi ya Ethiopia siku ya kesho kutwa Novemba 16 ugenini mchezo utakaochezwa nchini Congo DRC.Mchezo wa kwanza wa kufuzu mashindano hayo uliochezwa Dar es salaam Benjamin Mkapa Stadium ulitamatika kwa suluhu ya kutokufungana 0-0.
Stars inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa kundi H ikiwa na alama zake 4 baada ya kucheza michezo minne ikishinda mechi moja ikitoka suluhu mechi moja na kupoteza michezo miwili mfululizo dhidi ya timu ya taifa ya Congo DRC.
Mchezo dhidi ya Ethiopia unabeba matumaini ya kufuzu kwa mashindano hayo, kama ikatokea Stars ikapoteza dhidi ya Wahabeshi nafasi ya kutinga kucheza michuano mikubwa kwa ngazi za taifa Afrika itakuwa finyu kwa mazingatio ya mchezo wa mwisho itacheza dhidi ya Guinea ambayo nayo inahitaji kushinda ili ijihakikishie tiketi yake ya kuelekea nchini Morocco.
Ethiopia inaonekana ni mpinzani ambaye ni rahisi kushinda mchezo dhidi yao hilo ni kosa kubwa kama Wachezaji wa timu ya taifa Tanzania wataingia uwanjani wakiwa na haya mawazo watajikuta muda unaenda wakishindwa kupata goli za mapema presha itakuwa kubwa kwao na kushindwa kufanya maamuzi yaliyo sahihi hivyo kupelekea kuondoka na matokeo ambayo hayatokuwa rafiki kwa taifa.
Mchezo wa kwanza uliochezwa Dar es salaam kila Mtanzania aliamini Stars ingeondoka na matokeo chanya kwenye mchezo ule lakini matokeo ya mwisho hayakuwa sawa na matarajio ya walio wengi.Mchezo wa mpira wa miguu ni mchezo wa mbinu na makosa kama Kocha wa Ethiopia akaweza kutengeneza mbinu nzuri ya kuizuia Tanzania inaweza pia kupata matokeo mazuri kwao ya kushinda au kutoka sare.
Tanzania imefuzu kucheza AFCON mara 3 katika historia yake miaka ya 1980,2019 na 2023.Kama tunahitaji kufuzu tena AFCON ya mwakani nchini Morocco Wachezaji wanatakiwa kucheza bila kuidharau timu ya Ethiopia,hawapaswi kucheza kwa presha na kutumia nafasi yoyote itakayopatikana kwa ufanisi mkubwa ili kuondoka na matokeo ya ushindi ugenini.
Kocha Hemed Morocco ameita Wachezaji wenye uzoefu timu ya taifa kuhakikisha timu inafuzu kucheza AFCON kwa mara ya nne.Saimon Msuva,Mbwana Samatta na Aishi Manula wameitwa ili kuongoza jahazi la timu ya taifa kwenye michezo miwili ya kufuzu AFCON iliyosalia dhidi ya Ethiopia Novemba 16 na Guinea siku ya Jumanne Novemba 19 mchezo utakaochezwa Tanzania Dar es salaam dimba la Benjamin Mkapa.