Tuesday , 12th Nov , 2024

TAKUKURU wilaya ya Bukombe mkoani Geita, imemfikisha mahakamani Rashid Musalika ambaye ni Afisa Mtendaji wa kata ya Runzewe Mashariki kwa tuhuma za kujipatia shilingi laki tatu kutoka kwa wafugaji wa ng'ombe ili aweze kuachilia ng'ombe zao zilizokuwa zimelisha kwenye shamba la mkulima.

Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Geita Azza Mtaita

Akizungumza na Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Geita Azza Mtaita, amesema mshtakiwa huyo alifikishwa mahakamani Oktoba 30, 2024 na kufunguliwa kesi ya jinai namba 30949/2024 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya wilaya ya Bukombe ambapo alisomewa mashtaka na wakili wa serikali mwandamizi wa TAKUKURU Chali A.Kadeghe.

Aidha mshtakiwa alikana shtaka na upande wa mashtaka uliieleza mahakama kuwa uchunguzi umekamilika hivyo inaomba tarehe ya kusomwa kwa hoja za awali.

Hakimu alitoa masharti ya dhamana kwa mshtakiwa kuwa na mdhamini mmoja ambaye atasaini fungu la dhamana ya shilingi milioni moja na mshtakiwa alitimiza masharti ya dhamana na hivyo alidhaminiwa.