Monday , 11th Nov , 2024

Klabu ya Yanga ya imetangaza kuhamia uwanja wa KMC Complex uliopo Mwenge Dar es salaam na kuachana na uwanja wa Azam Complex Chamazi iliokuwa ukiutumia siku za nyuma.

Sababu mbalimbali zimetajwa juu ya uamuzi uliochukuliwa na Uongozi wa timu hiyo kuhamia uwanja wa KMC Complex ikiwemo picha za vidio ambazo hazina uthibitisho kama kweli zinaihusu klabu hiyo zikionyesha mabomba ya sindano uwanjani Azam Complex ikisemekana Wachezaji wake wanaongeza nguvu kwa kuchoma sindano.

Kuna hujuma nyingine mbalimbali zikitajwa kama sababu zilizofanya Wananchi kuamua kuhama uwanja. Kocha wa timu hiyo naye ametajwa kuwa sehemu ya tatizo lililopelekea Yanga kupoteza michezo miwili mfululizo.

Kiburi na kutokushaurika kwake kumepelekea timu kuambulia vipigo hivyo kutoka kwa timu za Azam na Tabora United, kitu pekee Yanga haipaswi kufanya ni kuruhusu kelele zisizo na msingi kuharibu hali ya utulivu iliyopo kwenye timu hiyo.

Watani wake wa Jadi Wekundu wa Msimbazi kikosi chake kimekosa ubingwa kutokana na kukosekana kwa utulivu pamoja na Wachezaji bora misimu mitatu mfululizo,kelele na kulaumiana hupelekea kupotea kwa morali ya timu na kuwagawa Wachezaji pamoja na Mashabiki hivyo kupeleka presha kwa timu nzima.

Uongozi wa Vilabu vyetu pendwa nchini mara nyingi hufanya maamuzi kwa mihemko kufata yanayosemwa na Mashabiki wa timu hizi kubwa za Kariakoo.Kuna kelele za Kocha hafai zimeanza kusikika mara Viongozi kukaa kikao kumjadili Mwalimu sitoshangaa kama mabingwa hao watetezi wakipoteza ubingwa wake kutokana na presha iliyopo kwasasa.

Kitu pekee wanapaswa kufanya ni kuangalia mapungufu ya kikosi chao yaliojionyesha kwenye michezo dhidi ya Azam FC na Tabora United ili kufanya vizuri kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya Al-Hilal S.C na baadae kukikabili kikosi cha Singida Big Stars FC siku chache mbele.

Kuna baadhi ya Wachezaji wa kikosi hiko chenye makao yake makuu mitaa ya Twiga na Jangwani wameshuka kiwango kutokana na kufanya starehe mmoja wao akiwa Mchezaji bora wa msimu uliopita Stephane Aziz Ki kiwango chake duni msimu huu kuzua mtafaruku kwa Viongozi na kugawanya Mashabiki wakisema kiwango chake kimechangia asilimia kubwa kuporomoka kwa timu hiyo.

Yanga haipaswi kushikana uchawi kwa sasa inapaswa kujadili chanagmoto zake na kuzitafutia ufumbuzi bila kupiga kelele kwa maana kadri wanavyozidi kunyosheana vidole ndivyo timu hiyo itakavyozidi kupoteza muelekeo kwenye ligi pamoja na michezo ya kimataifa.