Sunday , 10th Nov , 2024

Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe linamshikilia dereva wa Toyota Rumio, yenye namba za usajili T.633 ECF Ombeni Sanga (30), mfanyabiashara na mkazi wa Mji mdogo wa Tunduma kwa kosa la kuendesha gari kwa uzembe kisha kuacha njia, kupinduka na kusababisha kifo kwa Askari WP.11725 Koplo Leokadia

Askari WP.11725 Koplo Leokadia

Taarifa hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Songwe SACP Augustino Senga.

"Ni kwamba Novemba 10, 2024 saa 8:15 usiku eneo la Old Vwawa, Tarafa ya Vwawa, wilaya ya Mbozi mkoa wa Songwe katika barabara ya Mbeya - Tunduma gari ya Ombeni Evarist Sanga akitokea Tunduma kuelekea Vwawa iliacha njia, kupinduka na kusababisha kifo kwa askari polisi namba WP.11725 Koplo Leokadia Nestory Mwenda, aidha, katika ajali hiyo, Askari mwingine namba WP.11533 Koplo Tabia alijeruhiwa na kwa sasa anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Songwe," imeeleza taarifa ya SACP Senga.

Aidha uchunguzi umebaini kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva kushindwa kulimudu gari kutokana na mwendokasi.