Thursday , 7th Nov , 2024

Katika kuhakikisha huduma za mawasiliano zinarahisishwa ikiwemo za kifedha , vocha na mawasiliano kwa ujumla, kampuni ya Mawasiliano ya Airtel Tanzania imezindua Duka kwenye kituo cha Reli ya Kisasa (SGR), ili kusogeza huduma kwa wasafiri, wafanyabiashara, wakazi pamoja na wageni wanaotumi

Akiongea mara baada ya uzinduzi wa duka hilo, mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa kampuni ya AIRTEL, Eliud Sanga anasema huo ni muendelezo wao wa kuhakikisha unarahisisha huduma za mtandao wao kwa wananchi.

"Hili ni duka letu la pili kufungu kwenye kituo cha SGR, la kwanza tulifungua Morogoro na leo tumefungua Dar es Salaam, kikubwa tunataka kuendelea kusogeza huduma kwa wasafiri wetu hata wawapo katikati ya safari waweze kupata huduma zetu", Eliud Sanga-Mwenyekiti Bodi ya Wakurugenzi AIRTEL.

 

Mkurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania, Masanja Kadogosa anasema duka hilo ni linaongeza thamani kwa shirika na kupunguza usumbufu kwa wateja huku mkurugenzi wa kitengo cha huduma kwa wateja Adriana Lyamba akielezea namna wananchi watakavyonufaika na huduma hizo.

"Unaweza kukata tiketi mtandaoni lakini Airtel ndio wanarahisisha wananci kufanya malipo kwa urahii zaidi, lakini pia watafanya miamala wengine hela za kutumia hawana na wakifika hapa watatoa au kuweka pesa", Masanja Kadogosa-Mkurugenzi Mkuu TRC

 

"Kitu pekee naweza kuwaambia wateja wetu tunawapenda na tutaendelea kuwasogezea huduma hawatakuwa na haja tena ya kuhangaika kutafuta hudma watazipata hapahapa lakini pia watatuma na kutoa pesa na kupata mtandao bomba kyupitia duka hili", Adriana Lyamba -Mkurugenzi Huduma kwa Wateja Airtel