Pichani ni Profesa Jay Na Fid Q
"Marehemu Mama yangu alikuwa anafanya kazi Mwanza so mimi nilikutana na Fid Q Mwanza akiwa mdogo sana, kwahiyo Fid Q nilikuwa nacheza naye kikapu na mimi nilikuwa nacheza kikapu (Basket Ball) zamani na nilikuwa vizuri sana,so miaka ya baadae nilikutana naye bado anachana lakini hajatoka kimuziki'' Amezungumza Professor Jay
"Fid Q alikuwa amekata tamaa ya kufanya muziki alikuwa na daftari lake la nyimbo anataka kulichana aachane na muziki abaki kupambana na shule,Fid Q ni mtu mwenye akili sana hata darasani alikuwa yuko vizuri,wakati anataka kulichana daftari (La nyimbo zake) ndio nikamwambia mimi mwenyewe nilikuwa kama wewe mpaka kufikia level ya kujaza uwanja wa mpira,hivyo hatua zako hapa ni chache kufikia unapopataka'' Amezungumza Professor Jay
"Hivyo nilimpa nguvu ya kurudi kwenye muziki baada ya kuniona mimi nimetoboa tukikumbuka tulikuwa tunatembea wote,tumekua wote lakini mimi nikatoboa kabla yake kwahiyo ikamrudisha njiani nakuweza kufanya muziki na kweli baadae akaja kutoa Nyimbo na zikamuonesha njia akatoboa naye akaja kuwa Star na sasahivi ni Mkongwe hivyo namshukuru watu kama hao wanaokumbuka fadhila'' Amezungumza Professor Jay