Sababu za kuondoka kwake kwenye kikosi cha Gunners hazijawekwa wazi habari kutoka vyanzo mbalimbali Uingereza zinasema Edu inawezekana anavutiwa kujiunga na mradi wa Mmliliki wa timu Nottingham Forest F.C. Bwana Evangelos Marinakis wa kuijenga Forest kuwa timu tishio EPL.Hivyo kumshawishi Mbrazil huyo kujiuzulu nafasi yake ndani ya Arsenal.
Mkurugenzi wa michezo wa Arsenal Mbrazil Edu Gaspar anatarajiwa kuondoka Arsenal baada ya kuwasilisha barua ya kuacha kazi kwenye Bodi ya Wakurugenzi wa klabu hiyo yenye mako yake makuu London kwa mujibu wa Daily Mail kiungo huyo wa zamani wa Gunners ataondoka katika klabu hiyo baada ya mazungumzo yanayoendelea na uongozi wa Arsenal.
Mshindi huyo mara mbili wa EPL ya kikosi cha Arsenal kilichoshinda taji la ligi ya Uingereza bila kupoteza mchezo 2004 alirejea klabuni hapo 2019 baada ya kucheza michezo 127 chini ya Arsene Wenger. Kazi yake katika dirisha la usajili imesaidia Arsenal kusajili wachezaji muhimu kama Martin Odegaard na Declan Rice na kuwaondoa wachezaji wenye majina makubwa kama Mesut Ozil na Aubameyang.
Sababu za kuondoka kwake kwenye kikosi cha Gunners hazijawekwa wazi habari kutoka vyanzo mbalimbali Uingereza zinasema Edu inawezekana anavutiwa kujiunga na mradi wa Mmliliki wa timu Nottingham Forest F.C. Bwana Evangelos Marinakis wa kuijenga Forest kuwa timu tishio EPL.Hivyo kumshawishi Mbrazil huyo kujiuzulu nafasi yake ndani ya Arsenal.
Edu alichangia kwa kiasi kikubwa Kocha Mikel Arteta kujiunga kwenye kikosi hiko, baada ya kuushawishi Uongozi wa The Gunners kumchukua Mhispania huyo kutoka Manchester City ambako alikuwa Mwalimu Msaidizi wa Pep Guardiola.
Kiungo huyo wa zamani wa Arsenal FC, Valecncia FC na Sport Club Corinthians Paulista amewahi kuhudumu kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Brazil tangu mwaka 2016 mpaka 2019 alipojiunga na Washika Mitutu wa London akiwa Mkurugenzi wa ufundi wa kwanza kwenye klabu hiyo.
Kuondoka kwake kunaweza kusababisha mmomonyoko ndani ya kikosi cha Mikal Arteta kwakuwa wamefanya kazi kwa pamoja muda mrefu, wamefanikiwa kujenga timu imara ambayo imerudisha furaha kwa Wana Arsenal wote Duniani kutokana na mwenendo wa timu kwenye ligi kuu Uingereza pamoja na ligi ya mabingwa barani Ulaya.