Sunday , 3rd Nov , 2024

Klabu ya Liverpool ya uingereza haikamatika kwenye muendelezo wa ligi hiyo baada ya jana kupata ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Brighton and Hove Albion . Ililazimika kutoka nyuma kushinda mchezo huo uliopigwa kwenye dimba la Anfield.

Matokeo hayo ya ushindi yameipaisha timu hiyo inayotokea Merseyside mpaka nafasi ya kwanza msimamo wa EPL baada ya kucheza michezo 10 ikiwa imejikusanyia alama 25 alama mbili zaidi ya kikosi cha Manchester City kinachoshika nafasi ya pili kilichojikusanyia alama 23.

Klabu ya Liverpool ya uingereza haikamatika kwenye muendelezo wa ligi hiyo baada ya jana kupata ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Brighton and Hove Albion . Ililazimika kutoka nyuma kushinda mchezo huo uliopigwa kwenye dimba la Anfield.

Matokeo hayo ya ushindi yameipaisha timu hiyo inayotokea Merseyside mpaka nafasi ya kwanza msimamo wa EPL baada ya kucheza michezo 10 ikiwa imejikusanyia alama 25 alama mbili zaidi ya kikosi cha Manchester City kinachoshika nafasi ya pili kikiwa na alama 23.

Timu hiyo inayonolewa na Arne Slot imepoteza mchezo mmoja tu wa ligi kuu msimu huu mpaka sasa dhidi ya Nottingham Forest F.C kwa goli 1-0. Chini ya uongzi wa Kocha raia wa Uholanzi kikosi cha Majogoo ya Jiji kinacheza mpira mzuri na kimejenga mazingira ya kucheza mpaka Refarii apulize filimbi ya mwisho ndipo mechi inakuwa imeisha kwa upande wa kikosi hiko. 

Nyota wa Misri Mohamed Salah anaonyesha kiwango kikubwa chini ya Slot akiwa anahusika kwenye kutengeneza na kufunga goli muhimu zinazoamua matokeo ya Liverpool kwa ujumla. Ameshafunga goli 7 kwenye michezo 10 ya EPL msimu huu.

Wachezaji ambao hawakuwa sehemu ya kikosi cha kwanza chini ya Jurgen Klopp na walikuwa wanatumika kama mbadala wa wengine wanapopumzishwa ama wanapopata majeraha chini ya Mkufunzi mpya wameonekana kuwa muhimu Ryan Gravenberch,Konstantinos Tsimikas na Cody Gakpo wanafanya kazi kubwa chini ya Arne Slot.

Kocha wa kikosi cha Majogoo ya Jiji la Liverpool alitanabaisha mbele ya Waandishi wa habari juu ya matamanio yake ya kushinda ubingwa wa kila kombe ambalo timu hiyo inashiriki msimu huu. inaongoza ligi kuu Uingereza, imefuzu kucheza hatua ya robo fainali kombe la Carabao na imekusanya alama 9 katika michezo mitatu ya ligi ya mabingwa barani Ulaya msimu wa 2024-2025. hakuna aliyetemea Liverpool FC ingekuwa kwenye kiwango bora baada ya kuondoka kwa Jurgen Klopp mwezi Julai 2024.