Friday , 1st Nov , 2024

Kocha wa Yanga Miguel Gamondi anapitia kipindi kigumu kwenye kikosi cha Yanga SC kutokana na ugumu wa ratiba ya Yanga SC kwenye michezo ya ligi kuu Tanzania bara huku kikosi chake kikiwa na Wachezaji majeruhi ambao muhimu kwake kulingana na aina ya uchezaji wa timu hiyo.

Kesho Novemba 2 Yanga itakuwa uwanjani kukabiliana na Azam FC kwenye muendelezo wa michezo ya ligi kuu Tanzania bara kuna wasiwasi timu hiyo  ikacheza mchezo huo bila Mabeki wa pembeni Yao Kuoassi na Shedrack Boka ambao ni majeruhi  Nickson Kibabage naye akiwa hatihati kutokana na kupata maoumivu kwenye mchezo dhidi ya Singida Black Stars.

Gamondi raia wa Argentina amesikika mara kadha akilalamikia ratiba ya ligi kutokuwa rafiki kwao klabu hiyo inatakiwa kucheza michezo 7 ndani ya siku 21 ukitafuta wastani wake ni mchezo mmoja ndani ya masaa 72. Juzi  mchezo  dhidi ya Singida Black Stars uliochezwa  uwanja New Amaan Stadium Zanziba ulisababisha majeruhi wapya kwenye kikosi cha Wanajangwani  Chadrack Boka alipata majeruhi ya kifundo cha mguu na kulazimika  kutokuendelea na mchezo.

 Nickson Kibabage naye alionekana kuchechemea kwenye mchezo huo ambao aliingia kutokea benchi kuchukua nafasi ya Boka. Yao Kuoassi Atoula alikosekana nafasi yake alicheza Denis Nkane, Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania bara ilipata matokeo ya ushindi wa goli 1-0 lililofungwa na Pacôme Zouzoua.

Kesho Novemba 2 Yanga itakuwa uwanjani kukabiliana na Azam FC kwenye muendelezo wa michezo ya ligi kuu Tanzania bara kuna wasiwasi timu hiyo  ikacheza mchezo huo bila Mabeki wa pembeni Yao Kuoassi na Shedrack Boka ambao ni majeruhi  Nickson Kibabage naye akiwa hatihati kutokana na kupata maoumivu kwenye mchezo dhidi ya Singida Black Stars.

Ratiba ya Ligi imekuwa ngumu kwa timu zinazoshiriki ligi kuu Tanzania bara msimu huu kutokana kukosekana kwa muda wa kupumzika Wachezaji na kulazimika kucheza kila baada ya siku tatu na timu nyingine zinasafiri ndani ya hizo siku tatu bila kupata mapumziko. Kuna hatari kubwa sana kwa Wachezaji kupata majeraha ya mara kwa mara kutokana na kutakiwa kuchezwa wakiwa na uchovu.

Kikosi kinachonolewa na raia wa Argentina Gamondi kinashika nafasi ya kwanza kikiwa na alama 24 baada ya kucheza michezo 8 ya ligi kuu ikiwa timu pekee msimu huu wa 2024-2025 ambayo haijaruhusu goli mpaka sasa na kesho itakuwa uwanjani kukabiliana na Azam ambayo ni Mpinzani wake kwenye mbio za ubingwa wa TPL.