Thursday , 31st Oct , 2024

Klabu ya Manchester United inatarajia kumtangaza Ruben Amorim kuwa Kocha wao mpya muda wowote siku ya leo baada ya kufikia makubaliano ya kuvunja mkataba wa Mkufunzi huyo kutoka timu yake ya Sporting Lisbon ya nchini Ureno. amesaini mkataba wa miaka miwili na miezi 18 utafikia tamati 2027.

Taarifa rasmi kutoka ndani ya makao makuu ya kikosi hiko inatarajiwa kutoka  muda wowote siku ya leo na Mreno huyo anatarajia  kuanza kusimamia timu hiyo kwenye mchezo wa ligi kuu Uingereza dhdi ya Ipswich Town utakaochezwa Novemba 24, 2024. 

Klabu ya Manchester United inatarajia kumtangaza Ruben Amorim kuwa Kocha wao mpya muda wowote siku ya leo baada ya kufikia makubaliano ya kuvunja mkataba wa Mkufunzi huyo kutoka timu yake ya Sporting Lisbon ya nchini Ureno. 

Mabosi wa Man U wamekubali kulipa zaidi ya shilingi bilioni 19 za Kitanzania ili kuweza kupata huduma za Mkufunzi huyo. Kilichokwamisha mazungumzo na kutangazwa kwa Amorim yalikuwa matakwa ya Lisbon kuhitaji fedha zaidi kwa ajili ya kuwaruhusu Watu wa benchi la ufundi ambao wanafanya kazi na Ruben.

Taarifa rasmi kutoka ndani ya makao makuu ya kikosi hiko inatarajiwa kutoka  muda wowote siku ya leo na Mreno huyo anatarajia  kuanza kusimamia timu hiyo kwenye mchezo wa ligi kuu Uingereza dhdi ya Ipswich Town utakaochezwa Novemba 24, 2024. 

Mkufunzi huyo raia wa Ureno mwenye miaka 39 inasemekana amesaini mkataba wa miaka 2 na miezi 8, kandarasi yake itafikia tamati 2027 na kuna kipengele cha kuongeza miezi 12 zaidi kama atafanya kazi ambayo Mabosi wa Mashetani wa Jiji la Manchester wataridhika nayo.

Ruud van Nistelrooy ataendelea kuiongoza Man U mpaka Novemba 11, 2024 baada ya hapo utawala wa Amorim utaanza ransi ndani ya Manchester. Kikosi cha Mashetani Wekundu kitaikaribisha Chelsea FC kwenye mchezo wa ligi kuu Uingereza siku ya Jumapili November 3, 2024 ligi itasimama kupisha michezo ya ligi ya mataifa ya Ulaya kuanzia Novemba 11.

Mabingwa wa EPL wa mwaka 2013, jana usiku walipata ushindi wa goli 5-2 dhidi ya Leicester City kwenye michuano ya kombe la Carabao mzunguko wa 4. Ushindi huo umeifanya klabu hiyo kuvuka kucheza hatua ya robo fainali na itakabiliana na Tottenham Hotspurs kwenye uwanja wa White Hart Lane hatua ya robo fainali ya mashindano ya kombe hilo.

Ruben Amorim atakuwa Meneja wa 6 kukiongoza kikosi hiko tangu Mkufunzi mwenye heshima kubwa ndani ya United Sir Alex Ferguson astaafu mwaka 2013, ambapo ilikuwa mara ya mwisho klabu hiyo  kushinda ubingwa wa ligi kuu Uingereza.