Monday , 28th Oct , 2024

Viongozi wa Dini mkoa wa Dar es Salaam, wametakiwa kuliombea Taifa ili liweze kuwa na viongozi wanaomjua Mungu ili wasije kuharibu kuvuruga uwepo wa nyumba za ibada.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila kwenye mazishi ya aliyekuwa Askofu wa Kanisa la Calvary, Nabii Jonathan Shemhambu iliyofanyika Kawe kwenye Kanisa la Arise and Shine Kawe jijini Dar es Salaam.

"Tunaposema mliombee Taifa tunamaanisha na viongozi waliopo kwani tukipata viongozi ambao hawaijui Dini wanaweza kuamka na kuamrisha makanisa yote yafungwe pamoja na Misikiti na hamna kitu mtapinga lakini mkiliombea Taifa tunapata viongozi walio bora na wanapenda wananchi wake wamjue Mungu." Albert Chalamila Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Kwa upande wake kiongozi wa Kanisa la Inuka Uangaze Mtume Boniface mwamposa pamoja na Mtume John Sekalala wanaelezea namna walifanya kazi kwa zaidi ya miaka 20 na marehemu.