Monday , 28th Oct , 2024

Msanii Zuchu ameamua kuwatolea uvivu wadau pamoja na mashabiki wa muziki Tanzania ambao wamekuwa wakimshindanisha msanii huyo na malkia wa bongo fleva Lady Jayde katika upande wa uandishi pamoja na utumbuizaji katika stages

Pichani Ni Zuchu na Lady Jaydee

Haya yote yametokana na performance aliyoifanya Komando siku ya jumamosi katika jukwaa la #BongoFlevaHonors ambapo mashabiki na wadau walianza kuwalinganisha wawili hao kwenye ufanyaji wao wa kazi.

Zuchu katika insta story yake amelitolea uvivu jambo hilo kwa kupost maneno haya......."Huu ni mjadala usio na mashiko na wa kijinga kuwahi kutokea'' Ameandika Zuchu.

"Lady Jaydee ni moja kati ya Role Models wangu nampa heshima kubwa sana sababu yeye ni moja kati ya mifano bora sana tuliyonayo kwenye tasnia especially mabinti, kunishindanisha mimi na dada zangu waliotengeneza njia kama dada komando ni kuivunjia heshima tasnia,nakomesha mijadala hii mara moja''