Friday , 25th Oct , 2024

Timu ya Wanachi inashika ya pili nyuma ya Singida Black Stars ikiwa imejikusanyia alama 18 katika michezo sita iliyocheza imefunga goli kumi na moja na haijaruhusu goli mpaka sasa kwenye ligi kuu ya Tanzania bara TPL.

Kocha mkuu wa Klabu ya Yanga Miguel Gamondi amesema ratiba ya Ligi Kuu ni ngumu kutokana na ukaribu wa michezo. Gamondi ameeleza hayo wakati mkutano na Waandishi wa habari kuelekea mchezo dhidi ya Coastal Unioni hapo kesho Oktoba 26 Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha.

“Nimefurahi sana kuwa Arusha tena, kiukweli tuna ratiba ngumu kidogo, tumejaribu kupangilia ratiba yetu tupate angalau muda wa kupumzika. Hatupaswi kulalamika isipokuwa kupambana na hali halisi, ingawa ukweli ni kwamba hii sio ratiba nzuri ya kujiandaa na mchezo”

Aidha Kocha Gamondi amesifu upana na utajiri wa kikosi chake kuwa unampa nafasi kubwa kutumia mfumo wowote bila kuathiri ufanisi wa timu.

“Yanga tuna utajiri mkubwa wa vipaji ambao unanipa wasaa wa kutumia mfumo wowote bila kuathiri ufanisi wa mchezaji mmoja mmoja. Ingawa mimi siamini sana kwenye mfumo  bali namna gani sahihi ya kutengeneza nafasi na kuzitumia. Nina mawasiliano mazuri sana na wachezaji wangu wote licha ya kwamba sio wote wanapata nafasi”-Miguel Gamond.

Yanga itashuka dimbani kesho ugenini dhidi ya Coastal Union kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid ikiwa na kumbukumbu ya ushindi kwenye michezo miwili iliyopita dhidi ya Simba SC na JKT Tanzania. Yanga ambao ni Mbingwa Watetezi wa taji la ligi kuu Tanzania bara haijaruhusu goli mpaka sasa katika michezo sita iliyocheza msimu huu wa 2024-2025.

Timu ya Wanachi inashika ya pili nyuma ya Singida Black Stars ikiwa imejikusanyia alama 18 katika michezo sita iliyocheza imefunga goli kumi na moja na haijaruhusu goli mpaka sasa kwenye ligi kuu ya Tanzania bara TPL.

Gamondi amelalamikia ratiba ya ligi kuu kutokana na kucheza kila baada ya masaa 72 hivyo kuwapa wakati mgumu benchi la ufundi kurekebisha makosa ya timu hapohapo Wachezaji wanapaswa kupumzisha miili kabla ya kuingi kwenye mchezo mwengine.

Mabingwa wa Tanzania wataingia tena uwanjani dhidi ya Singida Black Stars Oktoba 30, itacheza na Azam Novemba 2, kutokana na ratiba ya michezo ya ligi kufuatana imempelekea Kocha mkuu wa timu ya Wananchi kuiongelea akiwa anazungumza na Waandishi wa Habari kuelekea mchezo wao dhidi ya Wagosi Wakaya.