Wednesday , 23rd Oct , 2024

Mkuu wa mkoa wa Arusha Paul Makonda ameagiza wakandarasi watakao chelewesha miradi ya maji mkoani humo waripotiwe ofisini kwake na watalala polisi kama hawatofata masharti ya mikataba waliyokubaliana.

Paul makonda ameyasema hayo wakati alipotembelea mradi wa maji wa uliopo Chekereni Mkoani Arusha ambao unatarajiwa kuzalisha maji lita million 220 za maji ambapo amewaagiza watendaji wa mamlaka ya maji (AUWSA) mkoani humo kuhakikisha wanasimamia miradi ya maji na inakamilika kwa wakati kama ilivyokubaliwa kwenye mkataba.

“Nyinyi watendaji wa Mamlaka ya maji wewe wa kijijini utakula spana mpka unyoke wewe wa mjini utanyooka nimalizie tuu nilikwambia siku ile mkurugenzi wa AUWSA mkandarasi yeyote atakayekuwa na kazi ya maji kwenye huu mkoa wa arusha akafanya kazi kwa namna anavyotaka asifate mkataba kwa sababu makata unampa muda tutamchukua tutamtafutia sehemu ya kulala central afanye kazi akitokea polisi” Amesema Paul Christian Makonda.

Aidha mkuu wa mkoa ameiagiza mamlaka ya maji mkoani humo kuandaa utaratibu wa gharama nafuu kwa kuwafungia maji wasio na uwezo wa kulipia gharama za kufungiwa kwa wakati mmoja kwa kuwafungia maji huku wakilipa gharama hizo kidogo kidogo huku wakiwa na huduma ya maji.

“Niwaombe kwa wale wananchi ambao hawana uwezo wa kulipia gharama za kuunganishiwa maji wekeni utaratibu wa kuunganishia mwananchi maji na atalipa taratibu inawezekana hana pesa ya kuunganishiwa kwa wakati mmoja mnaweza mkamuunganishia maji alaf akawa analipa kwenye bili yake ile kidogo kidogo” Amesema Paul Makonda.