Wednesday , 23rd Oct , 2024

Familia ya Lebron James imefikia rekodi iliyowekwa na  Familia ya Ken Griffey aliyecheza na Mtoto wake  Ken Grifey JR  uwanja mmoja kwenye timu ya Seattle Mariners michezo ya ligi ya kikapu Marekani msimu wa 1990-1991, walicheza kwa pamoja michezo 51.

Mfungaji bora wa muda wote wa NBA LeBron James usku wa jana Oktoba 22, 2024 aliweka rekodi nyingine  kwenye ligi ya kikapu Marekani maarufu NBA. King aliweka rekodi ya  kuchangia uwanja na mwanawe LeBron ‘Bronny’ James Jr mwenye umri wa miaka 20 kwenye mchezo uliozikutanisha  LA Lakers dhidi ya Minnesota TimberWolves  waliposhinda vikapu 110 kwa vikapu 103.

Wawili hao baba na mwana waliingia kortini kwa wakati mmoja katika mechi yao ya ufunguzi wa msimu dhidi ya Minnesota Timberwolves kwenye uwanja wa Crypto.com Arena kwa shangwe kutoka kwa  mashabiki wao ambapo Bronny alifanikiwa kufunga alama  kwa dakika tatu, huku LeBron akifunga alama 16 na  kuisaidia Lakers kupata ushindi katika mechi hiyo ya ufunguzi. 

LeBron Junior Bronny alijiunga na Los Angels Lakers mwezi Juni 2024, akiwa ni chaguzi ya pili kutoka  Chuo Kikuu cha Southern California. 

Lebron James amecheza Ligi kuu ya kikapu Marekani kwa miaka 22 na amezitumikia timu tofauti kwa kipindi chote hiko. Nyota huyo kwa sasa ana umri wa miaka 39 amesaini mkataba mpya wa miaka miwili zaidi kusalia kwenye timu yake ya Los Angels Lakers baada ya Mtoto wake kujiunga na mabingwa wa NBA wa mwaka 2020.

Lebron bingwa  mara 4 wa NBA, ameingia mara 20 mfululizo kwenye NBA all stars pia ni mshindi mara 4 wa tuzo ya MVP.