Tuesday , 22nd Oct , 2024

Dada wa msanii Diamond Platnumz Esam Platnumz ameamua kumshauri msanii kutoka label ya The African PrincessYammi Tz kuwa ni muimbaji mzuri lakini kitu kinacho muangusha ni performance zake stejini.

Pichani Ni Esma Platnumz na Yammi

Esma Ameyasema hayo katika insta story yake ambapo ameandika..........."Yammi mdogo wangu unaimba vizuri mno ila mashabiki zako unatuangusha kwenye stage unapooza sana embu mtafute Angel Nyigu akupike,anayekwambia ukweli siku zote anakupenda"

Esma amefunguka hayo ikiwa ni siku kadhaa tu zimepita tangu msanii huyo (Yammi) atumbuize katika jukwaa la Tanzania Music Awards ambapo kwa mujibu wa Komenti za mashabiki na wadau mbalimbali wa muziki walionesha kutopendezwa na utumbuizaji wake siku hiyo.