Monday , 21st Oct , 2024

Wakili wa kiongozi maarufu wa upinzani nchini Msumbiji Elvino Dias, ameuawa kwa kupigwa risasi katika Mji Mkuu wa Maputo wakati akiwa na mmoja wa afisa wa chama chake. 

Elvino Dias alikuwa wakili wa Venâncio Mondlane, ambaye aligombea urais katika uchaguzi siku kadhaa zilizopita kama mgombea binafsi akiungwa mkono na chama cha siasa cha Podemos.

Dias alikufa akiwa na afisa wa Podemos Paulo Guambe wakati watu wenye silaha waliposhambulia gari lao.

Shirika lingine la waangalizi wa uchaguzi wa Mais Integridade, lilisema mauaji hayo yalipangwa ili kumtisha mtu yeyote anayedai uwazi katika uchaguzi.

Inaelezwa kuwa, Dias alikufa papo hapo, huku Guambe, akifariki kwa majeraha masaa machache baadaye. 

Tukio hilo limetokea Oktoba 19 mwaka huu