Friday , 18th Oct , 2024

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe Albert John Chalamila, amecheza namba 9 katika mchuano mkali Kati ya timu ya Ofisi ya Mkoa na Shule ya Sekondari Kijitonyama ndani ya dakika 90 na kuibuka kidedea ambapo shule ya Sekondari ushiriki katika mechi maalum ya mpira wa miguu iliyofanyika katika

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila akipambana na vijana wa Shule ya Sekondari Kijitonyama.

Katika kuendeleza na kukuza michezo mbali mbali mkoani Dar es salaam, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh John Albert Chalamila amewataka wakuu wa wilaya kuunda timu za ofizi za wilaya ili kuwe na kongamano maalum la michezo mbali mbali kati ya timu za ofisi ya wilaya, Mkoa na taasisi za elimu.

Bonanza Hilo maarufu kwa jina 'Chandimu Challenge' limefanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Kijitonyama Kisiwani lililolenga kuwa sehemu ya kampeni ya kuhamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, ambao unatarajiwa kufanyika hivi karibuni Tarehe 27/11/2024.

Vilevile kupitia mtanange huo uliohusisha mpira wa kikapu  washindi kutoka Ofisi ya Mkoa walioiibuka kwa mabao 44 huku upande wa timu ya Shule ya Sekondari wakiambulia bao 5 tu. Mwisho wa michezo kupitia michuano hiyo washindi wa kwanza upande wa netball walipata kombe  na pesa taslimu shilingi laki 500,000 huku washindi wa pili wakipata shilingi laki 250,000 na makombe sawa na washindi wa football.

Mwisho, bonanza hilo lilihudhuriwa na viongozi mbalimbali ikiwemo Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, walimu, wanafunzi,na wadau wengine.