Thursday , 17th Oct , 2024

Didie Gomes Da Rosa ni Kocha mwenye uzoefu mkubwa na mpira wa Afrika, alishawahi kushika nafasi ya tatu katika tuzo za Zarpa Awards Makocha bora wa Kifaransa waliopo Afrika mwaka 2015, Al Ahly Tripoli imemuajiri Da Rosa baada ya kumfuta kazi raia wa Tunisia Chokri Khatoui.

Kocha wa zamani wa klabu ya Simba amesaini mkata wa kuitumikia timu ya Al Ahly Tripoli ya nchini Libya. Didie Gomes Da Rosa alikuwa akifundisha timu ya taifa ya Botswana kabla ya kujiuzulu nafasi yake na kutangazwa kwenye klabu hiyo ya Libya kuwa Kocha wao mkuu. Gomes raia wa Ufaransa alishinda taji la ligi kuu Tanzania bara, kombe la shirikisho Tanzania ( FA ) na aliiwezesha klabu ya Wekundu wa Msimbazi kucheza hatua ya robo fainali kombe la klabu bingwa Afrika msimu wa 2021.

Klabu ya Al Ahly ya nchini Libya kupitia mitandao yao ya kijamii imemtangaza Didie Gomes Da Rosa kuwa Kocha wao mkuu baada ya kumfuta kazi raia wa Tunisia Chokri Khatoui. Didie Gomes aliwahi kuifundisha timu ya Simba SC ya Tanzani kwa mwaka mmoja na kuiongoza  klabu hiyo kushinda kombe la ligi kuu Tanzania bara, kombe la shirikisho Tanzania ( FA ) pia aliiwesha timu hiyo kucheza robo fainali ya ligi ya mabingwa Afrika msimu wa 2020-2021.

Kocha huyo raia wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 55, ameajiriwa na Tripoli ya Libya ili kuweza kuiongoza timu hiyo baada ya  kushindwa kufuzu kucheza hatua ya makundi ligi ya Mabingwa barani Afrika ambapo   iliondoshwa mashindanoni na klabu ya Wekundu wa Msimbazi kwa kufungwa goli 3-1 katika uwanja wa Benjamini Mkapa Jijini Dar es salaam.

Al Ahly Tripoli ilifanya usajili mkubwa katika dirisha kubwa lililopita la usajili kwa kumuongeza kwenye kikosi chao Mshambuliaji wa tinu ya taifa ya Angola  Cristovao Paciencia Mabululu,  kushindwa kwao kufuzu kucheza hatua ya makundi mashindano klabu bingwa Afrika imetajwa kuwa ni sababu kubwa ya kuajiriwa kwa Didie Gomes Da Rosa ili kuisaidia timu hiyo kufanya vizuri kwenye mashindano ya ndani ya Libya na mashindano ya CAF kwa msimu ujao wa 2025-2026.

Didie Gomes alikuwa akifundisha timu ya taifa ya Botswana kabla ya kutangaza kujiuzulu nafasi yake muda mchache tu baada ya kukiongoza kikosi cha The Zebra kushinda mechi ya nyumbani na ugenini dhidi ya Cape Verde michezo ya kufuzu michuano ya AFCON 2025 itakayofanyika nchini Morocco.

Kocha huyo anayefahamika kwa uwezo wake mkubwa wa kubadilika kimbinu, anauzoefu mkubwa wa mpira wa Afrika baada ya  kuhudumu kwenye timu mbalimbali za Vilabu Afrika kama Simba SC ya Tanzania, Rayon Sports ya Rwanda, Coton Sports ya nchini Cameruni Ismaily na El Merrikh SC.