Amesema katika dunia ya sasa kwenye sanaa ndiko kuna uwanja mkubwa wa ajira
Simbachawene ametoa kauli hiyo leo Oktoba 12, 2024 wakati akizungumza kwenye mahafali ya 15 ya kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Kinyerezi iliyopo katika Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salam
"Nimefarijika kuona vipaji vya kila aina, nimewaona wasanii wenye vipaji vikubwa na pia nimeambiwa kuna mwanafunzi kwa sasa yupo Uingereza alichukuliwa tu mara baada ya kuhitimu masomo yake kutokana kipaji kikubwa alichonacho cha kucheza mpira " amesema .Simbachawene
Amesema makuzi ya mrengo wa kisasa kwa wanafunzi wa sasa ni jambo lisiloepukika kwa vile wanafunzi walio wengi wanaohitimu masomo yao hawarudi vijijini kulima
Kufuatia hatua hiyo Mhe.Simbachawene amewataka wahitimu hao wa kidato cha nne na wanafunzi wanaoendelea na shule licha ya vipaji walivyonavyo wajitahidi kusoma kwa bidii huku akiwasisitiza kujiepusha kuiga tamaduni za kigeni ambazo haziendani na tamaduni zetu.
Katika hatua nyingine, Mhe.Simbachawene amempongeza Rais Mhe.Samia Suluhu Hasssan kwa kukubali kutoa kiasi cha Sh. Bilioni 28 kwa ajili ya jiji la Dar es Salaam ili ziweze kutumika kwenye ujenzi wa madarasa
Amesema Serikali ya awamu ya tano imedhamiria kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu kwenye mazingira bora na ya kisasa ili kuhakikisha hakuna mtoto anayeachwa nyuma katika kutimiza ndoto zake
Awali, Mkuu wa Shule hiyo, Daniel Mwaka amesema Shule hiyo licha ya kuwa nyumba ya vipaji lukuki lakini kwenye suala la ufaulu wa masomo imekuwa ifanya vizuri mwaka hadi mwaka
Amesema katika kipindi cha miaka mitatu mfululizo, ufaulu wa wanafunzi umekuwa ni zaidi ya asilimia 80 na kusisitiza kuwa ufaulu wa wahitimu wa mwaka huu ufaulu utapanda zaidi hadi kufikia asilimia 93 kutokana na jinsi wanafunzi hao walivyoandaliwa.