Friday , 11th Oct , 2024

Ronaldo ndiye Mchezaji aliyefunga goli nyingi zaidi Duniani pia anashikilia rekodi ya kufunga goli nyingi zaidi kwenye timu za taifa kwa muda wote mpaka sasa ameshaifungia timu ya taifa ya Ureno goli 132 akiwa amewazidi Lionel Messi 109 na Ali Daei wa Iran mwenye goli 108.

Nahodha wa timu ya timu ya taifa ya Ureno ameitumikia timu hiyo michezo 214 akifunga goli 132. Akiwa amedumu kwenye timu hiyo mabingwa wa ubingwa wa mataifa ya Ulaya UEFA EURO 2016,kwa miaka 20 Ronaldo ndiye Mchezaji bora wa Ureno wa muda wote mbele ya Eusebio na Luis Figo japo kwa sasa Mashabiki wanataka apumzike apishe damu changa

Mashabiki nchi Ureno wapiga kura  kumkataa Cristiano Ronaldo kwenye mpango wa timu hiyo Wakisema uwepo wake unawanyima Wachezaji Vijana wanaocheza nafasi yake kupata nafasi kwenye  kikosi cha timu ya taifa lao. Kwa mujibu wa matokeo ya kura zilizopigishwa na kituo cha Habari cha CNN nchini Ureno Mashabiki   asilimia sabini na nne (74% )   hawamtaki Nahodha wao kikosini. 

Roberto Martinez raia wa Hispania ambaye ndiye Kocha wa timu ya taifa Ureno amesema yeye ataendelea kumtumia nyota huyo kutokana na ushahidi wa data ambao ni siri unaonyesha ni jinsi gani Mchezaji huyo amekuwa muhimu katika mipango yake.

Wadau wa soka nchini Ureno Wanasema katika goli 10 alizofunga Nahodha wa Ureno hivi karibuni  7   amefunga dhidi  timu ambazo zipo nje ya hamsini bora kwenye orodha ya shirikisho la mpira Duniani FIFA. 

Ronaldo amelitumikia taifa lake kwa miaka ishirini akifanikiwa kucheza fainali tatu za mashindano makubwa akiwa na jezi ya Mabingwa wa kombe la Mataifa ya bara la Ulaya wa mwaka 2016, Akifanya hivyo katika fainali za mwaka  2004 ambazo Ureno ilkuwa mwenyeji  ilipoteza mchezo wa fainali dhidi ya Ugiriki, Fainali ya pili 2016 dhidi ya Ufaransa ilifanikiwa kutwaa ubingwa kwa kuifunga timu hiyo ambayo ilikuwa mwenyeji wa mashindano,Ureno ilishinda  kombe la ligi ya Mataifa ya Ulaya mwaka 2019   baada ya kuifunga  Uholanzi kwa goli 1-0. 

Nyota wa Al Naseer ya nchini Saudi Arabia anapambana kuweka rekodi ya kuwa Mchezaji aliyefunga goli 1000 Duniani, kwa sasa amefikisha idadi ya goli 900 alizofunga akiwa na klabu za Sporting Lisbon ya Ureono 5, Manchester United Uingereza 145, Real Madrid Hispania 450, Juventus 101, timu ya taifa  Ureno 132, AL Naseer 68 jumla amefunga goli 901 kwenye mechi za mashindano rasmi.

Mchezaji huyo  tuzo bora wa Dunia mara 5 anatarajia kuiongoza timu ya taifa Ureno ugenini dhidi ya Poland siku ya Jumamosi Oktoba 12 kwenye muendelezo wa michezo ya ligi ya mataifa ya bara la Ulaya.