Thursday , 10th Oct , 2024

Kwenye mahojiano yake mwaka 2018 na CNBC aliulizwa unatamani Dunia imkumbuke Ratan Tata kwa kitu gani, alijibu kwa kusema ''Kwa haraka kabisa, kama nilivyokwisha kusema hapo awali, natamani kukumbukwa kama mtu aliyetengeneza utofauti na si zaidi ya hapo na si chini ya hapo''

 

Ratan Tata ni mfanyabiashara mashuhuri kutokea nchini India na aliyewahi kuwa mwenyekiti wa Tata Group, moja ya makampuni makubwa zaidi nchini India. Aliongoza kampuni ya Tata kutoka mwaka 1991 hadi 2012, na chini ya uongozi wake, kampuni hiyo ilipanua shughuli zake kimataifa kwa kununua kampuni nyingine kama vile Jaguar, Land Rover na Tetley Tea ambazo zote zilikuja kuwa chini ya kampuni ya Tata

Ratan Tata Pia ni mfadhili wa miradi mbalimbali kwenye jamii, akiwa kama mtu aliyejitoa kwa hali na mali kwenye sekta ya elimu, afya, na maendeleo ya vijijini.

Oktoba 9, 2024 akiwa anapatiwa matatibabu kwenye hospitali moja wapo huko kusini mwa Mumbai, alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 86 huku taarifa za awali zikisema ni changamoto za umri na shinikizo la damu.