Wednesday , 9th Oct , 2024

Kuelekea mchezo wa Dabi ya Kariakoo utakaozikutanisha timu za Simba na Yanga beki kisiki wa timu ya Simba amekiri Wapinzani wao ni bora na wana Wachezaji bora kwenye maeno mengi ndani ya uwanja, Che Malone ameyasema hayo siku ya jana Oktoba 8, 2024 kwenye Media Day iliyofanyika Bunju

Beki wa Simba Che Malone Fondo amezungumzia mchezo wa dabi Oktoba 19, 2024 dhidi ya Yanga kwa kusema Wapinzani Wao wanaubora maeneo mengi ndani ya uwanja hivyo kufanya mechi baina yao kutokua rahisi, Che Malone ni mmoja wa Wachezaji wa kutumainiwa kwenye kikosi cha Wekundu wa Msimbazi anafahamu umuhimu wa kushinda mchezo huo kwani wakipoteza watakua wamefungwa kwenye mechi nne mfululizo dhidi ya Yanga

Beki wa kutumainiwa wa timu ya Simba SC klabu siku ya jana Oktoba 8, 2024 kwenye Media Day iliyofanyika Bunju ulipo uwanja wa mazoezi wa Wekendu wa Msimbazi alizingumzia mchezo ujao wa tarehe Oktoba 19,2024 dhidi ya Watani wao wa jadi timu ya Yanga unaofahamika kama dabi ya Kariakoo.

Che Malone raia wa Cameroon ambaye amekuwa kipenzi cha Mashabiki wa timu hiyo yenye makao yake makuu mtaa wa Msimbazi Kariakoo amesema anafahamu ubora wa Wapinzani wao hivyo haitokua mechi rahisi kwao. Simba imepoteza michezo mitatu mfululizo dhidi ya Watani wao  wapo kwenye presha kubwa kuhakikisha wanapata matokeo ya ushindi dhidi ya Yanga.

Mlinzi kisiki aliyetengeneza safu imara ya ulinzi na Abdulrazack Hanza kwenye kikosi kinachofundishwa na kocha Fadlu Davids mpaka sasa wameruhusu goli mbili pekee katika michezo mitano ya ligi kuu Tanzania bara msimu huu.

Beki huyo anayesifiwa kwa kucheza kwa kujituma muda wote awepo uwanjani amekiri ubora wa Yanga na kusema wanapaswa kujiandaa kimwili na kiakili kama wanataka kuwafunga Yanga kwenye dabi ijayo. Pia amezungumzia jinsi gani anapenda kucheza kwenye michezo mikubwa yenye presha kama mchezo dhidi ya Watani wao wa jadi.

''Mara nyingi nimekua nikisema Yanga wanakikosi imara sana,wanapokua uwanjani nia yao huwa ni kushinda nchezo hivyo tunapswa kujiandaa,mpira wakati mwengine unamaajabu yake ikiwa hiyo siku ilibidi ufungwe basi utafungwa ila mapenda kucheza mechi kubwa zenye presha kama hizi

"Tunapaswa kukubali mechi yetu dhidi ya Yanga ni kama fainali, itaonesha kesho yetu ilipo, ni mechi ngumu sana inahitaji maandalizi mazuri  kiakili ili tuweze kushinda kwakuwa haijawahi kua mechi ya kawaida.

Simba imeimarisha kikosi chao kwa kuongeza Wachezaji kama Leonel Ateba, Debora Fernandes, Yusufu Kagoma na Abdulrazak Hamza ambao wanatoa matumaini makubwa kwa Mashabiki wa Mnyaka kushinda mchezo wa dabi utakaochezwa Oktoba 19, 2024 kwenye uwanja wa Benjamini Mkaba jijini Dar es salaam