Geoge Mugale, mkazi wa Dar es Salaam
Wameyasema hayo ikiwa leo makampuni mbalimbali nchini yanaadhimisha wiki ya huduma kwa wateja iliyoanza leo Oktoba 7 mpaka 11 na kuyaomba makampuni kuendeleza huduma hiyo hata baada ya wiki ya huduma kwa wateja kuisha.
Geoge Mugale, mmoja kati ya watu waliofika katika moja ya Duka la Vodacom walilokuwa wanatoa zawadi kwa wateja wao ameipongeza kampuni hiyo ambayo kwa sasa umepiga hatua kubwa sana katika upatikanaji wa mtandao kwenye kila kona nchini pmoj na Application ambazo zimekuwa zikitusaidia kupata huduma mbalimbali.
Nae Fatma Rajabu wakala wa Vodacom ameomba changamoto za kimtandao ziweze kushughulikiwa ili kupunguza changamoto kwa wananchi.
Harieth Rwakatali ambaye ni Mkurugenzi ni Mkurugenzi wa huduma kwa wateja amewakaribisha wateja wa Vodacom kufika kwenye maduka ya Vodacom kujipatia ofa mbalimbali ambazo wanazitoa katika wiki ya huduma kwa wateja.
Aidha Rwakatali amewatoa hofu wateja wa Vodacom kuhisi kuwa huduma hizi zitaishia wiki ya huduma kwa wateja peke yake bali ni utaratibu wa kampuni hiyo kutoa huduma bora kwa wateja wake.