Ajali ya mabasi mawili iliyotokea jijini mbeya alfajiri ya leo
Watu kadhaa wanahofiwa kufariki dunia na wengine kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha mabasi mawili ya kampuni ya Kapricon Express inayofanya safari ya kusafirisha kutoka Mbeya kwenda Jijini Arusha na Premier Line inafanya safari ya kusafarisha abiria kutoka Mbeya kwenda Mwanza kugongana uso kwa uso eneo la Sae kata ya Ilomba jijini Mbeya
Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo wameeleza chanzo cha ajali ni gari dogo lililotokea eneo la Mbeya Pazuri Social Club kata ya Ilomba Jijini Mbeya kuingia barabarani bila kuchukua tahadhari na kusambabisha mabasi hayo kutafuta jinsi ya kulikwepa gari hilo na kugongana EATV itakuleta taarifa kwa undani zaidi.