Wednesday , 25th Sep , 2024

Beki wa zamani wa Real Madrid, Manchester united na timu ya taifa ya Ufaransa Rafael Varane ametangza kustaafu kucheza soka leo Septemba 25, 2024 akiwa na umri wa miaka 31. Amestaafu kutokana na majeraha ya goti.

Majeraha ya mara kwa mara ndio sababu iliyomfanya beki huyo wa kati astaafu kucheza soka, baada ya kupata majeraha ya goti mwezi uliopita akiwa na timu ya Como ya Ligi kuu Italia Serie A ambayo alijiunga nayo mwanzo mwa msimu huu akitokea Manchester United.

Kwa ujumla Varane ameshinda makombe 21 ngazi ya klabu ikiwemo ubingwa wa Ligi ya mabingwa Ulaya UEFA Champions League akiwa na Real Madrid, pia ameshinda kombe la Dunia mwaka 2018 akiwa na timu ya taifa ya Ufransa na ubingwa wa UEFA Nations League. Amecheza zaidi ya michezo 570 kwenye maisha yake ya soka.