Tuesday , 24th Sep , 2024

Kwenye hali ya kukabiliana na changamoto nzito kwenye maisha, inafikia kipindi inakuwa ni ngumu sana kwako kufanya maamuzi kwa hofu ya kwamba huenda maamuzi yasiwe sahihi au yakaleta matokeo ambayo hukuweza kuyatarajia.

 

Suzy Welch ambaye ni muandishi wa vitabu na mshauri wa masuala ya kibiashara, alikuja na kanuni nyepesi ili kumsaidia mtu yeyote pale ambapo atahitaji kufanya maamuzi kwenye jambo lolote.

Kanuni ya Suzy Welch inafahamika kama; (10/10/10 rule)  ikiwa imebeba maana ya kwamba kabla ya kufanya maamuzi yoyote kwenye maisha fikiria kwenye jambo hilo dakika 10 zijazo litaleta matokeo gani?, miezi 10 ijayo maamuzi yako yataleta matokeo gani? na miaka 10 ijayo yataleta matokeo gani?

Lengo la kuja na kanuni hii, ni kuangazia tathimini ya matokeo kwenye maamuzi utakayo fanya kwa sasa, muda kidogo na wakati ujao.

Vipi hii kanuni unaweza kuitumia kwenye maisha yako?