Monday , 23rd Sep , 2024

Mwenyekiti wa Simba SC Murtzan Mangungu amesema licha ya kupata ushindi wa bao 3 - 1 dhidi ya Al Ahly Tripoli ya Libya lakini amekiri kuwa wapo kwenye hatua ya kujenga timu katika msimu huu wa kimashindano 2024- 2025

Akizungumza na waandishi wa Habari Mwenyekiti Mangungu amewataka mashabiki waendelee kuiunga mkono timu yao katika kipindi hiki ambacho wamefanya usajili mkubwa . 

''Tangu awali ujenzi wa timu ni wa hatua kwa hatua inayoendelea kwasasa pale tunapoona tunacheza tukiona mapungufu tunyafanyia kazi '' amesema Magungu. 

Nao mashabiki wa klabu za Simba SC na Yanga wamezipongeza timu zao zilizofanya vizuri katika michezo ya kimataifa na kupelekea kutinga makundi ya mashindano ya CAF . 

Kikosi cha Simba SC kimekuwa kinatinga makundi kwa mara ya sita ndani ya misimu saba ya michuano yote ya CAF ngazi za klabu, lakini hii ikiwa ni mara ya pili katika michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika baada ya msimu wa 20210 2022 ilipokwamia robo fainali

Vilevile Yanga ametinga makundi ya ligi ya mabingwa Afrika kwa kishindo kwa msimu wa pili mfululizo ikiwa ni historia kwa klabu hiyo katika michuano hiyo CAF na sasa inasubiri kujua itapagiwa na vigogo gani hatua hiyo mara baada ya kufanyika kwa droo Oktoba 7, 2024.