Kushoto ni Mwenyekiti wa CHADEMA Freemani Mbowe na kulia ni aliyekuwa Mjumbe wa Sekretariati ya chama hicho Taifa, Ali Mohamed Kibao
Mbowe ametoa kauli hiyo hii leo Septemba 8, 2024, wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufanyika kwa uchunguzi wa mwili wa Kibao katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa ya Mwananyamala.
"Postmortem imeshafanyika na ni dhahiri kwamba Ali Kibao ameuawa, baada ya kupigwa sana na hata kumwagiwa tindikali katika uso wake, mwili sasa hibi unaandaliwa ili taratibu nyingine za kifamilia ziweze kuendelea," amesema Mbowe
Aidha Mbowe ameongeza kuwa "Sisi kama chama tunaendelea kufanya mashauriano pamoja na familia ili katika hatua za baadaye tuone tunaweza kuchukua hatua gani za kisheria kwa sababu mtu huyu ameuawa na hatuwezi kuruhusu hali hiyo ikaendelea," - Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa.