Thursday , 5th Sep , 2024

Kaimu Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stras Hemed Suleiman amewaomba watanzania wawe wavumilivu na timu yao, kwani timu hiyo ipo kwenye kipindi cha mpito ikiwa inaundwa na wachezaji vijana zaidi.

Kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania ''Taifa Stars" kimetoka suluhu dhidi ya Ethiopia jana, mchezo wa kufuzu AFCON 2025.

Kocha Hemed Suleiman amesema hayo baada ya kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania taifa Stars kutoka suluhu 0-0 dhidi ya timu ya taifa ya Ethiopia kwenye mchezo wa kundi H wa kuwania kufuzu fainali za AFCON 2025. Mchezo uliocheza jana Usiku katika dimba la Benjamini Mkapa.

“Hii timu ipo kwenye kipindi cha mpito wachezaji wengi ni vijana hivyo wanahitaji muda, ukitazama wachezaji wote. Hiki ni kipindi cha mpito kwenye timu yetu ya taifa tunahitaji kuwapa moyo wachezaji wetu ili kuhakikisha wanacheza vizuri.” Amesema Hemed Suleiman

Taifa Stars itashuka tena Dimba Septemba 10, 2024. Itakuwa ugenini kucheza mchezo wa pili wa hatua hii ya makundi dhidi ya timu ya taifa ya Guinea. Mchezo mwingine wa Kundi H la taifa Stars utachezwa kesho ambapo Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo watakuwa wenyeji wa Guinea.