Wednesday , 28th Aug , 2024

Wanawake nchini wametakiwa kuachama na dhana potofu na kuchangamkia nafasi za Uongozi kwenye chaguzi zijazo za nchi yetu ili kuweza kupata usawa kwenye ngazi za juu za Uongozi.

Dorothy Temu, Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo

Hayo yamesemwa na kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo Dorothy Temu, leo jijini Dar es Salaam wakati anaongea na EATV, kuhusu umuhimu wa mwanamke kuwania nafasi ya uongozi.
“Kwanza waachane na dhana potofu mwanamke anaweza na ana nguvu na uwezo wa kuongoza jamii, niwahamasishe wanawake na mabinti kutumia chaguzi zijazo kuleta mabadiliko kwenye jamii yetu”, alisema Temu.

 

Kwa upande wake Naibu Katibu Ngome ya Vijana ACT Wazalendo anaelezea umuhimu wa vijana wa kike kugombea Uongozi.
“Wanawake wengi hasa vijaana tunaona Uongozi sio sehemu yetu ndio maana tunaachwa nyuma sana hasa kwenye maamuzi lakini tukiwa kwenye nafasi tunaweza kupata nguvu ya kutetea hoja zilizobeba maslahi yetu”, alisema Rukaiya Nasry.

Nao baadhi ya mabinti wanaelezea shahuku yao ya kugombea kwenye chaguzi zijazo.
“Nimegundua wengi tupo nyumba lakini mwaka huu na mwaka ujao na ahidi kutangaza nia ili na mimi niwe miongoini mwa wanawake watakaoleta mabadiliko kwenye jamii”, alisema Sevelina Mola, Mwanachama wa ACT Wazalendo.

“2019 niligombea uenyekiti wa Mtaa Makumbusho nikakosa lakini mwaka huu narudi tena kwa nguvu na ahidi nitagombea kwa uwezo wa Mungu nitapata na nitatetea nafasi niliyoikosa”, Zawadi Mohamedi, Mwanachama ACT Wazalendo.