Tuesday , 27th Aug , 2024

Kiungo wa PSG ya Ufaransa Manuel Ugarte atasafiri leo Agosti 27-2024 kuelekea nchini Uingereza kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya Afya kujiunga na Manchester United kwa ajili ya msimu mpya wa mashindano 2024-25.

(Kiungo wa PSG Manuel Ugarte)

Ugarte mwenye umri wa miaka 23 ameichezea PSG kwenye michezo 37 huku alijiunga na miamba hiyo ya Paris akitokea Sporting CP ya Ureno mwaka 2023 ilhali usajili huu unakuja baada ya United kupanga kumuuza kiungo wake Scott McTominay kwenda SSC Napoli ya Italia kwa ada ya uhamisho wa Euro Milioni 30 sawa na zaidi ya Bilioni 90.5 kwa fedha za Kitanzania

Tayari PSG na Manchester United wamekubaliana ada ya uhamisho ya Euro Milioni 50 sawa na zaidi ya Bilioni 150.8 kwa fedha za Kitanzania kwa ajili ya kupata huduma ya kiungo kutoka Uruguay Manuel Ugarte.