
(Kiungo Mshambuliaji Cole Palmer)
Cole Palmer aliweka rekodi ya kuwa mchezaji aliyehusika kwenye mabao mengi zaidi kwenye EPL msimu uliopita 2023-24 baada ya kuhusika kwenye mabao 33 huku alifunga mabao 22 na kutoa pasi za usaidizi wa magoli mara 11.
Ilhali kwenye upande wa Fantasy League, Cole Palmer ni mchezaji wa 5 kwa kukusanya alama nyingi msimu huu akiwa na alama 19 tofauti ya alama 5 dhidi ya kinara Mo Salah wa Liverpool mwenye alama 24.