Wednesday , 21st Aug , 2024

Promota wa masumbwi Barry Hearn amesema kuna uwezekano mkubwa kwa pambano la masumbwi la uzito wa juu duniani baina ya Waingereza wawili Anthony Joshua na Tyson Fury linaweza kufanyika mwanzoni mwa mwaka 2025

(Bondia Anthony Joshua akiwa Ulingoni)

Barry Hearn anayetoka kampuni ya Matchroom ambao wamekuwa wakimsimamia Joshua tangu aingie kwenye ngumi za kulipwa amesema "pambano baina ya Aj dhidi ya Fury linaweza kufanyika mwanzoni mwa mwaka 2025 na kwamba watafanya kila linalowezekana kwa pambano kuweza kufanyika mwakani".

Anthony Joshua anataraji kupambana na Daniel Dubois kugombea mkanda wa uzito wa juu duniani wa IBF kwenye dimba la Wembley nchini Uingereza mnamo Septemba 21-2024 huku Tyson Fury atacheza pambano la marejeano dhidi ya Oleksandr Usyk kugombea mikanda ya WBA, WBO na WBC mnamo Desenba 21-2024.