Washtakiwa
Wakili Ngamando amesema mashahidi kwa siku ya leo walikuwa watano lakini kutokana na muda ni shahidi mmoja pekee ndiye aliyewezwa kusikilizwa.
"Kesi inasikilizwa vizuri na hakuna shida yoyote, wananchi tuwe na utulivu tusikilize kesi nina imani kwamba haki itatendeka," amesema Wakili wa upande wa utetezi.
Waliofikishwa mahakamani katika kesi hiyo ni askari wa JWTZ MT.140105 Clinton Damas maarufu kama Nyundo, askari Magereza C.1693 Praygod Mushi, Lord Lema na Nickson Jackson.
Kesi hiyo ya ubakaji kwa kikundi na kumlawiti binti wa Yombo Dovya jijini Dar es Salaam itaendelea tena kesho Agosti 21, 2024, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Dodoma.