Tuesday , 20th Aug , 2024

Maboresho ndani ya Uwanja wa Benjamin Mkapa uliopo Jijini Dar es Salaam yanazidi kushika kasi huku ukarabati huo ukitaraji kumalizika ndani ya kipindi kilichopangwa cha kimkataba baina ya Serikali na kampuni inayosimamia maboresho ndani ya uwanja huo.

Kaimu Meneja wa Uwanja wa Benjamin Mkapa ,Milinde Mahona amesema maboresho yanakwenda vizuri huku wamepunguza matumizi ya uwanja kwa kufanya matukio machache ili kusaidia kukamilika kwa haraka maboresho ndani ya uwanja huo

 "Tumefikia pazuri kwenye ukarabati wa uwanja wa Mkapa, Kama unavyoona hali ya uwanja inaendelea vizuri tofauti na siku kadhaa zilizopita na Matumizi ya uwanja yamepungua, Simba na Yanga, walikuwa wanatumia uwanja huu kama uwanja wao wa nyumbani kwenye mechi za ligi kuu, Timu nyengine sa nje ya nchi na Azam pia huwa wanatumia Kwenye baadhi ya mechi, ila kwa sasa tumepunguza matumizi hayo" Kaimu Meneja Uwanja wa Mkapa

Kwa upande mwingine,Milinde Mahona ameendeleza wito kwa mashabiki kuendelea kutunza miundombinu ya uwanja ili kusaidia uwanja huo kutumika kwa muda mrefu na kuepuka marekebisho yasiyokuwa ya lazima ndani ya uwanja huo

"Hatujapokea changamoto yeyote ya uharibifu wa uwanja, niendelee kuwaomba mashabiki wa soka wawe makini kuutunza uwanja wetu".