Friday , 16th Aug , 2024

Timu ya Vital O ya Burundi imetamba kuondoka na ushindi kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza wa ligi ya mabingwa barani Afrika 2024-25 dhidi ya Yanga SC utakaofanyika kwenye dimba la Azam Complex Chamazi mnamo Agosti 17-2024 Jijini Dar es Salaam.

Akizungumzia kuhusu matayarisho yao kwa ajili ya kuwakabili Yanga SC,Kocha msaidizi wa Vital O ya Burundi Sahabo Parris amesema wamejiandaa vyema kuwakabili Yanga huku amekiri kuwafatalia Yanga kwenye michezo waliyocheza hivi karibuni.

"Nimewasoma Yanga kupitia michezo yao waliyoicheza hivyo nitatumia mbinu ambazo zitaisaidia timu yangu iweze kupata ushindi katika mchezo huo, amesema Parris.

Wakati huo huo,Afisa Habari wa kikosi cha Yanga SC Ally Shabaan Kamwe amesema kuelekea mchezo wa Vital O ya Burundi wanakwenda kuweka  heshima na ubora wa Yanga ndani ya Afrika ya Mashariki na Kati na kuwaomba mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuipa sapoti timu yao.

"Malengo yetu ni kushinda na kwenda hatua inayofata tunakila sababu ya kushinda mchezo huo kutokana na ubora wa kikosi chetu hivyo waYanga wasijtokeze kwa wingi''amesema Kamwe.

Yanga SC ilimaliza hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa barani Afrika msimu 2023-24 kwa kuondolewa na Mamelodi Sundwons ya Afrika Kusini kwa changamoto ya mikwaju ya penati 3-2.