Wednesday , 14th Aug , 2024

Mwanariadha wa kimataifa wa Tanzania Alphonce Felix Simbu amesema anajipanga kwa ajili ya mashindano mengine yanayokuja ya riadha baada ya kushindwa kupata medali kwenye michezo ya Olimpiki ya Paris iliyomalizika Agosti 11-2024 nchini Ufaransa.

Akizungumza mara baada ya kuwasili nchini akitokea Ufaransa,Simbu ambaye alikuwa nahodha wa Tanzania kwa Wachezaji waliokwenda kushiriki kwenye michezo ya Olimpiki amesema changamoto kubwa ya kutokufanya vyema ni njia ya kukimbilia iliyokuwa na miinuko na mitelemko mikali iliyomkwamisha kutwaa medali ndani ya michezo hiyo ya Olimpiki 2024.

''Hizo njia za kukimbilia tulionyeshwa tu mitandaoni baadaa kufika nchini Ufaransa lakini hiyo imepita tunajipanga katika mashindano mbalimbali tumejifunza makosa''amesema Simbu

Kwa upnde mwingine,Wadau wa michezo nchini wamezungumzia kiufundi sababu zilizokwamisha Wanariadha 4 kutoka Tanzania kushindwa kutwaa medali kwenye michezo ya Olimpiki ya Paris mwaka 2024.