Saturday , 10th Aug , 2024

Mechi ya ufunguzi wa ligi kuu soka nchini Uingereza EPL, inachezwa leo Agosti 10,2024. Ni Mchezo wa ngao ya jamii kati ya Manchester City dhidi ya Manchester United unatarajiwa kuchezwa katika uwanja wa Wembley jijini London majira ya saa 11 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.

Kiungo wa Manchester united Casemiro wa kulia ni sehemu ya wachezaji watakao ukosa mchezo dhidi ya Man City kutokana na Majeraha.

Kuelekea mchezo huu timu zote mbili zina kabiliwa na majeruhi ya wachezaji wake muhimu, Manchester City itamkosa kiungo wake mshambuliaji Mahiri Jack Grealish ambaye anasumbuliwa na jeraha la mguu, huku habari njema ni kurejea kwa Kevin De Bruyne ambae ameanza mazoezi siku tatu zilizopita toka apate jeraha la paja mwishoni mwa msimu ulilopita.

 

Kwa upande wa Manchester united, Kocha Erik Ten Hag anakabiliana na changamoto za majeruhi ya wachezaji wake muhimu akiwemo Casemiro, Harry Maguire, Luke shaw na leny yoro. Hata hivyo habari njema kwa mashabiki wa United ni kwamba Mshambuliaji Marcus Rashford anatarajiwa kurejea kikosini na kuimarisha safu ya ushambuliaji mara baada ya kupona majeraha madogo aliyoyapata mwishoni mwa msimu ulilopita