Friday , 2nd Aug , 2024

Robert Ndiragoo (43) mkazi wa Kitongoji cha Mbeli Kijiji cha Kimana wilayani Kiteto mkoani Manyara amemuua mke wake kwa kumkata na kitu chenye ncha kali shingoni huku chanzo kikitajwa ni mtuhumiwa kutaka mahindi kwa nguvu.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara RPC George Katabazi amethibitisha kifo hicho na kumtaja marehemu kwa jina la  Joyce Jackson Mwanangombe (30), ambapo wakati akitekeleza unyama huo mtoto wao mwenye umri wa miaka 8 alishuhudia.

 

Tazama video ya mtoto huyo akisumilia namna ambavyo baba alivyomchoma kisu mama yake shingoni.